Video: Alichokisema Rais Magufuli Baada ya Kuwasili Kenya
akipokea shada la maua
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Balozi Amina Mohamed
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (kulia) akisalimiana na Magufuli.
Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride, Ikulu Nairobi, Kenya.
Uhuru Kenyatta akimtembeza Magufuli ndani ya Ikulu ya Kenya.
… Akisaini kitabu cha wageni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na
mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Baada ya kuwasili katika Ikulu ya Kenya jijini Nairobi, Rais Magufuli amekagua gwaride la heshima na kupigiwa mizinga 21
Akizungumzia mambo atakayoyafanya,
Msemaji wa Rais Kenyatta, Manoah Esipisu, Jumapili aligusia mambo ambayo
Kenya inatarajia kutoka kwa ziara ya Rais Magufuli nchini Kenya.
Alisema: “Ziara ya Rais huyu inatupatia
fursa ya kufanya upya na kukoleza uhusiano wetu katika nyanja
mbalimbali. Viongozi wa nchi hizi watashauriana kuhusu masuala
mbalimbali ya pamoja katika ngazi ya taifa kwa taifa na kanda.
Wataangazia sana masuala ambayo tayari kumekuwa na mazungumzo, na
tunatarajia matokeo ya mazungumzo hayo kutangazwa.
“Masuala kadha yatajadiliwa, ikiwemo ada
ya vibali vya kufanyia kazi ambayo raia wa Kenya hutozwa, pamoja na
karo ya juu ambayo Wakenya hutozwa vyuo vikuu (Tanzania). Mashauriano
kuhusu kuondoa vikwazo vya kibiashara baina ya nchi hizi mbili pia
yatafanyika. Kadhalika, na muhimu sana katika mazungumzo hayo ni
shughuli za magari ya kusafirisha watalii yanayovuka mipaka.
“Muhimu katika mashauriano haya itakuwa
pia kufufuliwa kwa Tume ya Ushirikiano wa Pamoja na Tanzania (JCC)
ambayo ni jukwaa ambalo linaweza kutumiwa kutangaza biashara na
uwekezaji baina ya nchi zote mbili.
“Rais Kenyatta pia atazungumza na Rais
Magufuli kumhusu Bi Amina Mohammed (waziri wa mambo ya nje wa Kenya)
anayewania wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.
Rais Magufuli akiwa Kenya atatembelea
kiwanda cha maziwa cha Eldoville kilichopo Karen Nairobi na kuzindua
barabara mchepuko jijini Nairobi.
VIDEO: Hotuba ya Rais Magufuli na Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuwasili Kenya
VIDEO: Hotuba ya Rais Magufuli na Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuwasili Kenya
Post a Comment