CHURA WA SNURA AFUNGULIWA.
Picha na Aviala Kakingo, Globu ya Jamii.
VIDEO mpya ya wimbo wa Msanii, Snura Mushi 'Snura' wa Chura ambao ulikuwa umefungiwa na Serikali, wimbo huo umefunguliwa na kuanza kuchezwa na kuoneshwa kwenye vituo vya Luninga pamoja na kupigwa kwenye vituo vya Redio.
Hayo yamesemwa na Msanii, Snura Mushi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa wimbo huo ameurekodia Video mpya yenye maadili ya Kitanzania na yenye staa zote na inaelezea maana halisi ya chura kama alivyomaanisha kwenye utunzi wa wimbo huo.
Post a Comment