BONDIA WA UZITO WA JUU TYSON FURY AKIRI KUBWIA UNGA AINA YA COCAINE
Bondia Tyson Fury amekiri kutumia
dawa za kulevya aina ya cocaine katika mahojiano marefu, ambayo
yamebainisha hali ya afya ya akili yake aliyokuwa nayo hivi sasa,
huku akisema kuwa kila siku anatarajia kufa.
Bondia huyo mwenye miaka 28 anahofia
mabadiliko yake ya tabia, ambapo hivi jumatatu aliandika kuhusu
kustaafu ngumi kwa kutumia akaunti yake ya twitta, na kisha baadaye
kuandika kuwa ulikuwa ni uongo.
Jumbe zake hizo katika mitandao ya
jamii zilifuatia uamuzi wa kujitoa kupigana Oktoba 29 kuwania mkanda
wa ubingwa wa dunia dhidi ya Wladimir Klitschko, ambalo liliharishwa
baada kuelezwa kuwa hayupo fiti kiafya.
Tyson Fury amekuwa akikabiliana na tatizo la msongo wa mawazo kwa muda sasa
Post a Comment