MANJI: MURO ANAENDELEA NA KAZI KAMA KAWA
Mwenyekiti wa Yanga,
Yusuf Manji (kushoto) akiongea jambo.
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, amevunja ukimya na kusema
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Jerry Muro yupo huru
na anaendelea na kazi zote za klabu kama kawaida.
Manji ameliambia Championi Jumatatu kwamba, klabu hiyo haina
taarifa yoyote rasmi ya kufungiwa kwa Muro.
“Kama taarifa tumesikia kwenye magazeti na redio, kweli
taasisi kama Yanga, msemaji wake anasimamishwa kwa njia hiyo?
“Hao waliomsimamisha pia ni taasisi, vipi
wafanye hivyo. Yanga tunawezaje kuamini hilo? Muro bado yuko kazini na
anaendelea na shughuli zake kama kawaida,” alisema Manji.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo,
Jerry Muro akifanya yake na mashabiki.
Manji amesisitiza kuwa kama ni kweli basi TFF inapaswa kutoa
hukumu ya kumfungia Muro kama ambavyo wamekuwa wakisikia.
TFF kupitia kamati ya nidhamu ilitangaza kumfungia Muro
mwaka mmoja ikiwa ni pamoja na kumpiga faini.
Lakini imekuwa ikisita kutoa hukumu yake inayohusiana na
Muro, jambo ambalo linaifanya Yanga kuona kuna upotofu wa mambo na kukiukwa kwa
usahihi.
Juhudi za gazeti hili kupata hukumu ya Muro zimekuwa
zikigonga ukuta hasa kutokana na kuhoji makosa yaliyomtia hatiani na viongozi
wa TFF wamekuwa wakisisitiza bado inaandaliwa jambo ambalo haliwezekani
kuchukua muda mrefu hivyo.
Post a Comment