Alichokisema Manji Baada Ya Taarifa Kuwa Kajitoa Yanga
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji (kushoto).
Baada ya taarifa kwamba Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji
amejiuzulu uenyekiti kuzagaa, SALEHJEMBE ilifanya kila juhudi kumpata
na mwenye akazungumza kwa ufupi.
Alipoulizwa kuhusiana na suala la kujiuzulu na pia
kusitiza uamuzi wake wa kutaka kuwekeza au kuikodisha Yanga kwa miaka
kumi, alisema basi imetosha.
“Kwa kweli imetosha, imetosha sasa,” alisema.
Alipoulizwa afafanue kuhusiana na kauli hiyo, Manji aliongeza.
“Nimesema hivi, imetosha. Naomba uniache, nisingependa kujibu lolote kwa sasa, niache tafadhari.”
Kumekuwa na taarifa kwamba Manji ameamua kuachana na
wazo lake la kuwekeza Yanga kwa miaka 10 baada ya kuona hata baadhi ya
viongozi wa serikali wakimuandama kwa madai wanatumiwa na baadhi ya
mamilionea.
Taarifa nyingine zimeelezwa kwamba, wako wanachama wa
Yanga ambao wanaona hawatafaidika na maslahi yao binafsi kama Manji
atawekeza, hivyo wamekuwa wakipambana kuhakikisha haingii mkataba na
kupewa nafasi hiyo kwa kuwa inaweza kuwavuruga.
Awali, kumekuwa na taarifa Manji ameamua kujitoa kwa
kuwa kuna juhudi za chini pia zinazohusisha hadi watu wengine wenye
mamlaka katika soka ambao wana hofu na uwekezaji wake.
CHANZO: SALEHJEMBE
Post a Comment