Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) waapa Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi
wa Polisi (SACP) na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya
Makamishna hao kula Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini
Dar es salaam leo.Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka
wasimamie utekelezaji wa Sheria bila woga na kuahidi kuboresha maslahi
ya Jeshi la Polisi nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) mara baada ya kula Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Naibu
Makamishna wa Polisi
(DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) wakifuatilia
kwa Makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli mara baada ya kula
Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) mara baada ya kula Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akiwaongoza Naibu Makamishna wa Polisi
(DCP) 35 na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) 23 kula
Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma mara baada ya kupandishwa vyeo na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Naibu Makamishna wa Polisi
(DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) wakila
Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma mara baada ya kupandishwa vyeo na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -
Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah
Kairuki ( kushoto)
akizungumza jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Eng.
John William Herbert Kijazi (wa pili kutoka kushoto)
Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya Naibu Makamishna wa
Polisi (DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) kula
kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma.Wengine ni Kamishna wa
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome
Kaganda na Inspekta Jenerali wa Polisi Ernest Mangu.
Katibu
Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja
Jenerali Projest Rwegasira
(wa pili kutoka kushoto)akizungumza jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju (kushoto)
leo Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya Naibu Makamishna wa
Polisi (DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) kula
kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma.Wengine kulia ni Waziri na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Kulia) na Mhe. Hamad Masauni.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali mara baada ya Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi
wa Polisi (SACP, Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali mara baada ya Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi
wa Polisi (SACP) kula Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini
Dar es salaam leo.Kutoka kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju,Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja
Jenerali Projest Rwegasira
(wa pili kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -
Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah
Kairuki ( kushoto), Kamishna wa
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome
Kaganda na Inspekta Jenerali wa Polisi Ernest Mangu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama leo Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi
wa Polisi (SACP).Picha/A.Msigwa.
Post a Comment