DIAMOND, VANESSA WASHINDA TUZO ZA 2014 AFRIMA HUKO NIGERIA
Vanessa Mdee akiwa na tuzo yake ya Best Female Artist in East Africa. |
Peter Msechu akiwa amebeba tuzo kwa niaba ya Diamond Platnumz.… |
MWANAMUZIKI
Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa kuamkia leo ametwaa tuzo ya
Mwanamuziki Bora wa Kiume Afrika Mashariki (Best Male Artist in East
Africa) kutoka Tuzo za 2014 AFRIMA zilizofanyika huko jijini Lagos
nchini Nigeria.
Mwanadada Vanessa Mdee yeye ameshinda tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika Mashariki (Best Female Artist in East Africa).
Tuzo
ya Diamond imepokelewa na mwanamuziki Peter Msechu aliyekuwepo katika
zoezi hilo la utoaji tuzo maana na yeye alikuwa kwenye kinyang'anyiro
cha kuwania tuzo hizo.
Post a Comment