Kivuko cha MV Kilombero kikiwa kazini.
ABIRIA wengi wamekwama katika eneo la Mto Kilombero mkoani Morogoro baada ya kivuko cha MV Kilombero kukwama kwa takribani saa 6 sasa.
Hakuna abiria wala gari lolote linalovuka katika eneo hilo hivyo kupelekea kuwepo kwa foleni kubwa ya magari kila upande wa mto huo.
Abiria eneo hilo bado hawajajua hatima yao mpaka sasa huku wakizitaka mamlaka husika kuwasaidia ili waweze kuvuka mto huo.
Post a Comment