DAKTARI ALIYESABABISHA VIFO VYA WATU 13 INDIA MBARONI

Dk. RK Gupta aliyetiwa mbaroni   
  .DAKTARI anayehusishwa na tukio la vifo vya watu 13 katika kituo cha kutoa huduma ya kuzuia uzazi kwa njia ya upasuaji jimboni Chattisgarh nchini India, Dk. RK Gupta ametiwa mbaroni.


Baadhi ya akina mama waliofanyiwa upasuaji wakiwa hospitali.
Dk Gupta na msaidizi wake waliwafanyia upasuaji wananawake 83 katika kijiji cha Pendari ndani ya saa 3 Jumamosi iliyopita na kusababisha vifo 13 huku wengi wakiwa wamelazwa hospitali, 20 kati yao wakiwa katika hali mbaya.
Raia wa India, Ram Avtar aliyempoteza mke wake aitwaye, Nem Bai akiomboleza na wanaye huko Bilaspur, Chattisgarh 
 Serikali nchini humo inamtaka daktari mmoja kutoa huduma ya upasuaji kwa watu 35 tu kwa siku.

No comments

Powered by Blogger.