TANZANIA YASHUKA NAFASI 6 VIWANGO VYA FIFA, BRAZILI YAONGOZA

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), leo Alhamisi limetoa viwango vya soka vya mwezi Julai kwa mataifa mbalimbali ambapo Tanzania imeshuka kwa nafasi sita kutoka 114 ya mwezi Juni mpaka 120.
Ikiwa duniani Tanzania inashika nafasi ya 120, kwa upande wa Afrika ipo ya 35, huku ikiwa ya nne katika Ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Uganda inaongoza ikifuatiwa na Kenya, kisha Rwanda na Burundi inaburuza mkia.
Katika nafasi 10 za juu kwenye orodha hiyo, Brazil inaongoza ikifuatiwa na Ujerumani, Argentina, Uswizi, Poland, Ureno, Chile, Colombia, Ubelgiji na Ufaransa inahitimisha.

No comments

Powered by Blogger.