MANJI APINGA MKOJO WAKE KUKUTWA NA MADAWA
Yusuf Manji (picha na maktaba)
KESI inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji ya kutuhumiwa na matumizi ya dawa za kulevya leo Ijumaa, Agosti 22, 2017 imeanza kutolewa ushahidi wa vipimo vilivyochunguzwa kwa mkemia mkuu wa serikali na majibu yake huku wakili wake akipinga kielelzo hicho cha mkojo hakikuwa halali.
Ushahidi huo umeanza kusikilizwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kwa nyakati tofauti shahidi wa kwanza alikuwa Ofisa Mkuu wa Makosa ya Jinai na Naibu Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam, Ramadhan Kindai na Askari Polisi Kitengo cha Upelelezi cha Makosa ya Jinai,
Wakifafanua mahakamani hapo wameeleza hatua zote walizozifuata tangu Manji aliporipoti Kituo Kikuu cha Polisi, Februari 9 mwaka huu na kupelekwa kwa mkemia kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo vya mkojo na hatimaye kugundulika anatumia madawa ya kulevya.
Kwa upande wa utetezi, Wakili wa Manji, Hoodson Ndusiepo aliukataa ushahidi wa barua iliyoandikwa ya Manji kupelekwa kwa Mkemia Mkuu ili kuchukuliwa vipimo vya mkojo kwa madai kuwa barua hiyo ilitakiwa kuwa na sahihi ya mteja wake kuridhia akachukuliwe vipimo hivyo.ristopher.
Pia wakili huyo alimhoji shahidi wa kwanza juu ya hati ya mashtaka iliyofunguliwa dhidi ya Manji inayoonesha mteja wake anatuhumiwa kwa matumizi ya dawa za kulevya aina ya Heroine na kwa nini inatofautiana na vipimo vya mkemia vinavyoonyesha aina ya madawa yaliyogundulika wakati wa vipimo kuwa aina ya Benzodiazepine.
Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkeha ameiahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano, Agosti 23.
Post a Comment