IGP Sirro: Mtu akihubiriwa ni rahisi kubadilika

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kulia) akizungumza na Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zubeir (kushoto), alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya BAKWATA jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, IGP Simon Sirro amesema ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na viongozi wa dini ni muhimu katika kudumisha amani na utulivu kwa sababu wao wana nafasi kubwa zaidi katika kuwabadilisha binadamu kiroho.
IGP Sirro amesema hayo wakati alipokwenda kumtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubary Bin Zubery Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam, na kusema mashirikiano hayo yanahitajika kwa ajili ya kudumisha amani na usalama wa nchi.
"Mufti wa Tanzania ni kiongozi wetu mkubwa upande wa imani ya kiislamu na kwenye suala zima la uhalifu katika kupambana na kuzuia uhalifu  yeye ana nafasi kubwa sana kwa sababu sisi tunafanya doria hizi za kibinadamu huku kuhakikisha tunazuia uhalifu lakini Mufti na timu yake wanafanya doria ya kiroho", alisema IGP Sirro.
Pamoja na hayo, IGP Sirro ameendelea kwa kusema "tunaamini doria ya kiroho ndiyo kitu kikubwa sana, mtu akishahubiriwa ni rahisi hata kubadilika hata usipotumia nguvu ya polisi kwa hiyo nimekuja kumsalimia kiongozi kwa kuwa ni muda mrefu hatujaonana. Tumezungumza  mambo mengi ya kiusalama na Mufti Mkuu ikiwemo suala zima na uhalifu katika wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani na ambapo kwa sasa hali ni shwari na amani imerejea kama ilivyokua awali na kuna maelekezo amenipa ya kutekeleza lakini kikubwa sisi ni kitu kimoja, tunahakikisha nchi yetu inaendelea na amani", alisisitiza IGP Sirro.
Kwa upande wake Mufti Zubery amesema dini inahusika moja kwa moja na jamii katika kuhakikisha suala zima la usalama wa nchi unapatikana 

No comments

Powered by Blogger.