DODOMA KUMENOGA, UCHAGUZI KILA KITU KIPO TAYARI, MRITHI WA MALINZI ANAJULIKANA

Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unafanyika leo mkoani Dodoma kwenye Ukumbi wa St Gasper kwa ajili ya kuwapata washindi wa nafasi ya urais, makamu wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji.
Uchaguzi huo unasimamiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Revocatus Kuuli unafanyika baada ya Jamal Malinzi kuelekea kumaliza kipindi chake cha uongozi cha miaka minne.
Wagombea wanaowania nafasi ya rais ni Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Fredrick Mwakalebela, Richard Shija, Emmanuel Kimbe na Ally Mayay Tembele.
Wanaowania nafasi ya makamu wa rais ni Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura na Mtemi Ramadhani.
Baadhi ya wagombea wa nafasi za ujumbe wa Kanda Namba 13 inayowakilisha Mkoa wa Dar es Salaam ni Emmanuel Kazimoto, Abdul Sauko, Ayoub Nyenzi, Shaffih Dauda, Peter Mhinzi, Lameck Nyambaya, Mussa Kissoky, Said Tully, Ally Kamtande, Aziz Khalfan, Ramadhani Nassib na Saad Kawemba.
Wagombea ujumbe wengine wa ujumbe Kanda Namba 9 inayowakilisha mikoa ya Lindi na Mtwara ni Athumani Kambi na Dunstan Mkundi. Kanda Namba 10 Dodoma na Singida wapo Hussein Mwamba, Steward Masima, Ally Suru na George Komba.
Kutoka Kanda Namba 1 inayowakilisha mikoa ya Kagera na Geita wanaogombea ni Salum Chama, Leopold Mukebezi na Kaliro Samson. Kanda Namba 2 Mara, Mwanza wagombea ni Aaron Nyanda, Vedastus Lufano, Samwel Daniel na Ephraim Majinge.

No comments

Powered by Blogger.