Diaspora kufanya Kongamano Zanzibar August 23 na 24
Watanzania wanaoishi nje ya nchi wametakiwa kuongeza juhudi katika hatua za kujenga nchi yao kwenye mambo ya maendelo ili nchi iweze kufikia malengo yake yaliyojiwekea kiuchumi na kijamii. Akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Issa Ussi Haji Gavu juu ya Uzinduzi wa kongamano la Diaspora linalotarajiwa kuzinduliwa tarehe 23 na 24 ya mwezi huu katika ukumbi wa baraza la wawakilishi la zamani.
Amesema ili Tanzania na Zanzibar iweze kuendelea kiuchumi na kijamii lazima wananchi washirikiane na serikali kikamilifu katika hatua mbalimbali za maendeleo.
Hata hivyo amesema mafanikio makubwa yameanza kuonekana kupitia michango ya watanzania wanaishi nje ya nchi hasa katika mambo ya maendeleo ikiwemo katika sekta za Elimu,Afya na miradi mengini ya kijamii jambo linaloleta faraja kwa wananchi.
“Watanzania wanaoishi nje ya nchi ni sehemu moja ya maendeelo hivyo hawana budi kuijenga nchi yao ili kuweza kulisukuma gurudumu la maisha mbele kimaendeleo”Waziri Gavu amesema.
Aidha Gavu amewataka watanzania kuzitumia fursa za uwekezaji nchini ili kuweza kutoa nafasi za ajira kwa vijana kuweza kuajiriwa ambapo itakuwa wameisaidia kwa kiasi kikubwa serikali katika mapambano la uhaba wa ajira.
Amefahamisha kuwa katika siku ya uzinduzi wa diaspora wafanyabiashara wa kibenki pamoja na wajasiriamali wataweza kupewa nafasi kuonesha huduma zao na biashara zao wanazozalisha.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Diaspora Adila Hilali Vuai ametoa wito kwa watanzania hao kuongeza bidii katika kuijenga nchi yao kiuchumi na kimazingira ili kuwa bora kimaendeleo kwani wao ni wadau wakubwa na wanahitajika katika kuendeleza taifa.
Amesema licha ya jitihada zinazochukuliwa na serikali kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali lakini bado Zanzibar kuna changamoto mbalimbali ambazo zinahiataji kupatiwa ufumbuzi ili maendeleo yaweze kupatikana kwa haraka.
Adila amesema kuna sekta kuu muhimu lazima ziungwe mkono mara kwa mara ikiwemo Elimu,Afya na huduma nyengine za kijamiii ili kuwasaidia wananchi wenye uhitaji na wanyonge wasiojiweza.
“Wakati umefika sasa wa kuipigania Zanzibar kufikia katika uchumi na maendeleo endelevu ili wananchi waweze kuneemeka na fursa za maendeleo”Amesema Mkurugenzi Adila.
Zaidi ya watanzania 350 kutoka nje ya nchi wanatarajiwa ushiriki kongamano la diaspore ambalo ni kongamano la 4 kufanyika nchini Tanzania.
Na:Amina Omar Zanzibar24
Post a Comment