OKWI: BOBAN NDIYE MCHEZAJI BORA KULIKO WOTE NILIOCHEZA NAO SOKA

Siku chache kabla ya kuanza kazi yake mpya ya kuitumikia Simba kwa mara ya tatu, mshambuliaji Emmanuel Okwi amezungumzia mambo kadhaa na kulitaja jina la Hauna Moshi ‘Boban’.
Akizungumza kuhusu msimu ujao wa 2017/18, Okwi kwanza alisema anafurahi sana kuwepo Tanzania kwa kuwa Watanzania ni watu wakarimu na ambao wamekuwa wakimtendea wema mara nyingi anapokuwepo hapa.

Kuhusu kombinesheni nzuri ambayo amewahi kucheza nao akiwa Simba, Okwi amesema anamkumbuka sana kiungo Haruna Moshi ‘Boban’ kutokana na mchango wake aliokuwa akiutoa wakati wakiwa pamoja Simba.

Okwi amesema Boban ni mchezaji bora kwake kuwahi kutokea kwa wachezaji ambao amecheza nao na ndiyo maana huwa hamsahau mchezaji huyo.

Aidha, amegusia juu ya ubora wa Felix Sunzu na Patrick Mafisango ambao alifanya nao kazi Simba kwa kusema kuwa walikuwa wakianya kazi nzuri.

Okwi amejiunga na Simba hivi karibuni akitokea Uganda wakati Boban kwa sasa yupo Dar es Salaam akiwa anacheza timu za chini.

No comments

Powered by Blogger.