Ngeleja Arudisha Mil. 40 za Escrow

                                                                         William Ngeleja 
Mbunge wa Sengerema kwa tiketi ya CCM, William Ngeleja amerudisha pesa kiasi cha Tsh milioni 40.4 alizohusishwa nazo kwenye sakata la Tegeta Escrow.

Pesa hizo inadaiwa kuwa alipewa mgao yeye na baadhi ya wabunge pamoja na viongozi wengine wa serikali, dini na majaji kutoka kwa James Rugemalira wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd.

Taarifa ya kurudisha fedha hizo ameitoa leo mbele ya waandishi wa habari ambapo alisema lengo la kuzirudisha ni kuhusishwa kwake na kashfa kuchotwa kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Ngeleja amedai kuwa fedha hizo alipewa msaada kama ilivyokuwa wabunge wengine waliogawiwa na James Rugemalira kwa ajili ya maendeleo ya jimbo lake la Sengerema na kusema licha ya kuwa fedha hizo zilikatwa kodi, ila amerejesha zote.
Hivi karibuni, TAKUKURU iliwafikisha mahakamni Kisutu, Harbinder Singh Sethi na James Rugemalila kwa makosa ya uhujumu uchumi.

No comments

Powered by Blogger.