Dar es Salaam. Hayawi hayawi sasa yamekuwa, ndivyo
unavyoweza kusema, baada ya Asha Abdallah maarufu Binti Dulla anayesadikiwa
kuwa na umri wa zaidi ya miaka 60, mkazi wa Mburahati Madoto kuolewa na Ally
Kimbunga (35) Ndugu katika familia ya bibi harusi, Hamisi Kondo alimwambia
mwandishi wetu kuwa hiyo ilikuwa ni ndoa ya nne kwa dada yake na kwamba,
waliomuoa awali walishafariki dunia. “Sasa hivi hana watoto, aliwahi kuwa na
mmoja ila ikawa si riziki kwa kuwa alifariki akiwa na miaka mitatu,” alisema
Kondo ambaye mama wa Binti Dulla ni shangazi yake. Kudra Saidi aliyewahi kuwa
mpangaji nyumbani kwa Binti Dulla kwa miaka 12 tangu 1990 ambaye alihudhuria
ndoa hiyo alisema majirani walipomfuata kuzungumza naye kuhusu kuolewa
aliwaeleza kuwa hata Mtume Muhammad (SAW) alioa mwanamke aliyemzidi umri. Kudra
alisema baadhi ya watu wamekuwa wakidai kwamba mume wa Binti Dulla amefuata
nyumba na kwamba mama huyo hana haja ya kupata mtoto. Hata hivyo, Binti Dulla
alisema maneno yanayozungumzwa kuhusu ndoa yake ni wivu wa baadhi ya watu
katika maisha aliyoyachagua. “Wazushi tena hao ni mashilawadu (wambeya) kwa
kuwa walijua sitafanikisha. Kuhusu suala la mtoto sina haja ya kupata mtoto kwa
kuwa nia yangu ni kuolewa na kuwa na mume, Mungu amefanikisha hilo,
Alhamdulillah Rabil-alamin,” alisema Binti Dulla. Binti Dulla alisema mama yake
hakufika kwenye ndoa yake kwa kuwa ni mgonjwa na anasumbuliwa na maradhi ya
moyo. “Mama yangu hakufika kutokana na hali yake na hayupo hapa anaishi Bagamoyo.
Juzi alitoka hapa kwangu alikokuwa akipatiwa matibabu, isingekuwa rahisi kwa
yeye kuja,” alisema. Akizungumzia ndoa hiyo mume Kimbunga alisema yeye si wa
kwanza kuoa mtu aliyemzidi umri. Alisema anamshukuru Mungu kwa hatua aliyopiga,
huku akisema wanaozungumza anawaacha waongee kwa kuwa ameshazoea. “Sikuanza
naye jana wala juzi, niko naye tangu mwaka 2007. Sijawahi kuoa na ndiyo mara
yangu ya kwanza na nimefuata maadili ya dini yangu na sunna ya Mtume Muhammad
(SAW) ambaye alioa mwanamke aliyemzidi umri,” alisema Kimbunga. Alisema
wanaodai yuko naye kwa ajili ya masilahi ni wazushi na kwamba, mke wake ni
mgonjwa wa kisukari tangu walipokutana na kama kumuacha angemucha kipindi cha
nyuma lakini wanapendana. Kimbunga alisema licha ya kuwa ni ndoa yake ya kwanza,
ana mtoto wa kike mwenye miaka 15 ambaye alikuwapo kwenye harusi. Alisema mama
yake anaishi Morogoro na kwamba, mzazi mwenzake hana shida juu ya yeye kuoa.
Jirani wa Binti Dulla (jina linahifadhiwa) aliyehudhuria ndoa hiyo na sherehe
hizo za siku mbili alisema ni vyema maharusi hao wangefunga ndoa kimyakimya
kutokana na umri wa mke
chanzo: mwananchi
Post a Comment