MGOMBEA URAIS TFF AJIPELEKA UHAMIAJI, AKABIDHI NYARAKA

Wakati mchakato wa uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukiwa kwenye harakati za kuendelea, imeelezwa kuwa mgombea nafasi ya urais wa shirikisho hyilo, Wallace Karia, leo Jumatatu alifika kwenye ofisiza Idara ya Uhamiaji.
Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu wa Karia ambaye pia ni kaimu rais wa TFF, zinaeleza kuwa Karia alifika kwenye ofisi hizo ili kukabidhi uthibitisho wa nyaraka mbalimbali kuhusu uraia wake.
“Amekabidhi kwa ajili ya wao wafanye uchunguzi lakini hakukaa sana, aliondoka na kuendelea na shughuli zake nyingine kama kawaida,” alisema mtu wa karibu wa mgombea huyo.
Hivi karibuni Karia aliwekewa pingamizi katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi ujao, ambapo ilielezwa kuwa si raia wa Tanzania lakini mwenyewe ameshajitokeza mara kadhaa na kupinga juu ya madai hayo akieleza kuwa yeye ni Mtanzania halisi.

No comments

Powered by Blogger.