MANJI ASOMEWA MASHTAKA AKIWA KITANDANI MUHIMBILI
Na Mwandishi Wetu: Wimbi la vigogo wa ngazi na hadhi mbalimbali kufikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali na kunyimwa dhamana limeendelea baada ya jana, mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji kusomewa shtaka la uhujumu na kunyimwa dhamana.
Jana mchana, waendesha mashtaka wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam, ilihamia katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako Manji amelazwa na kusomewa mashtaka saba, ambayo kukutwa na kukutwa na bidhaa visivyo halali, ambavyo ni vitambaa vyenye thamani ya shilingi milioni 44, ambavyo ni mahususi kwa ajili ya kutengeneza sare za JWTZ.
Wamekutwa na mihuri miwili ya JWTZ wa kwanza ni wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, Muhuli wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na mhuri mwingine wa Commanding Officer Korogwe, plate number 2 za magari ya serikali yanayowakabili washtakiwa wanne akiwemo Manji.
Pia washtakiwa wamekutwa na shtaka la kukutwa na mihuli ya Jeshi la Wananchi Kambi ya Makutupola, Dodoma Kambi namba 834 jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mtu mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja na watuhumiwa wote wamenyimwa dhamana.
Post a Comment