BREAKING NEWS: TUNDU LISSU APANDISHWA KIZIMBANI

                                     Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Baada ya kuwekwa mahabusu kwa siku nne, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki,  Tundu  Lissu leo amefikishwa Mahakama ya Kisutu kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Lissu alikamatwa, Alhamisi, Julai 20 mwaka huu, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)  wakati akijiandaa kuelekea Kigali, Rwanda  kwenye kikao cha Chama cha Wanasheria cha Afrika Mashariki (EALS).

Siku iliyofuata (Ijumaa), taarifa zilieleza kuwa polisi walikwenda kupekua nyumbani kwake na kuchukua iPad na CD na baadaye alipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kupimwa mkojo ambapo inaelezwa kuwa alikataa kwa madai kuwa kosa alilokamatwa nalo la uchochezi haliendani na kipimo cha mkojo.

No comments

Powered by Blogger.