Mtu Mmoja Akamatwa Akiingiza Nyama Zikiwa na Smart Phones 5 Kwa Wafungwa Gereza la Keko

 Mtuhumiwa Ramadhani Nombo akiwa amebeba mapande ya nyama ambayo yanatuhumiwa kuwa na simu tano ndani yake 

 DAR: Kijana mmoja amekamatwa leo akijaribu kuingiza simu 5 katika Gereza la Mahabusu Keko. Alizifungasha kwenye mapande ya nyama.
 Simu hizo zilikuwa ziingizwe gerezani humo ili wapewe wafungwa kwa ajili ya mawasiliano jambo ambalo ni kinyume cha sheria.


 Mtuhumiwa Ramadhani Nombo akiwa amebeba mapande ya nyama ambayo yanatuhumiwa kuwa na simu tano ndani yake 

 Jeshi  la Magereza jana Jumapili limemkamata kijana mmoja aitwaye Ramadhani Nombo akiwa na simu
tano alizozificha kwenye mapande ya nyama aliyokuwa ameletea ndugu zake walio
mahabusu katika gereza la mahabusu la Keko jijini Dar es salaam.


Kwa mujibu wa taarifa za jeshi hilo, hivi sasa vyombo vya
ulinzi na usalama vinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha
mahakamani mtuhumiwa huyo.


“Kutokana na umakini wa askari wetu mara alipofika na kuomba
kuwaone ndugu zake walio mahabusu na kuwapa chakula walibaini kwamba ndani yake
kuna simu” imesema taarifa hiyo. Haikutajwa nyama na hizo simu alikuwa
anapalekewa  mahabusu gani hapo gerezani.


Taarifa zinasema kimsingi kijana huyo amevunja Kifungu cha
86 (1) cha Sheria ya Magereza sura ya 56 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002
ambayo inakataza mtu yeyote kuingiza magerezani kitu chochote kisichoruhusiwa.


Kifungu hicho kinatamka bayana kwamba endapo ikithibitika
mtu yeyote amekamatwa na kuingiza kitu chochote ambacho hakiruhusiwi kuingizwa
gerezani, atahukumiwa kifungo kisichozidi miezi sita (6) gerezani au faini au
vyote kwa pamoja.

No comments

Powered by Blogger.