RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AKABIDHI UENYEKITI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KWA RAIS MUSEVENI
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kwa kukabidhiwa kiti cha jumuiya hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kiti cha jumuiya hiyo katika mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda baada ya kumkabidhi kiti cha jumuiya hiyo katika mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017
Wakuu wa nchi za Jumuiya ya afrika Mashariki wakisaini makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa katika mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017
Sehemu ya mawaziri na viongozi wengine wakishangilia wakati Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kiti cha jumuiya hiyo katika mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda baada ya kumkabidhi kiti cha jumuiya hiyo katika mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017
Picha na IKULU
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika mkutano huu wakati wa kukabidhi kiti cha Uwenyekiti amesema katika kipindi cha miaka miwili ya Uwenyekiti wa Tanzania, Jumuiya ya Afrika Mashariki imepata mafanikio makubwa na kuifanya istawi zaidi katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara kutokana na kupunguzwa kwa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiforodha, kuboreka kwa mfumo wa elimu ya Juu ndani ya Jumuiya na kuongezeka kwa Sudan Kusini katika Jumuiya.
Aidha, mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akiongea mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo amesema kuna kila sababu ya kulinda na kudumisha mtangamano uliopo kwa kuwa unaharakisha kasi ya maendeleo ya nchi wanachama na watu wake, unaimarisha ulinzi na usalama wa nchi wanachama, na kudumisha undugu wa kihistoria uliodumu kwa muda mrefu miongoni mwa nchi wanachama.
Mkutano huo pia umeshuhudia viapo vya viongozi wapya wawili katika ngazi ya Jumuiya ambao ni Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Sudan Kusini, Jaji Charles Oyo Nyawezo na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mrote kutoka Tanzania.
Post a Comment