Mmiliki wa shule ya Lucky, Waandishi 10 na Meya wa Jiji la Arusha Watiwa Mbaroni
Mmiliki
wa Shule, Meya wa jiji la Arusha pamoja na waandishi wa habari 10
wamefikishwa kituo cha polisi (Central) kwa kufanya mkusanyiko bila
kibali ndani ya shule ya Lucky Vicent.
Kutoka
Arusha taarifa zinasema kuwa Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Arusha (jina
lake halijafahamika) amedai kuwa kosa ambalo wamelifanya waandishi
pamoja Wamiliki ni kufanya mkusanyiko bila kibali ambao ni kinyume cha
sheria.
Vyanzo
vya habari vinadai kuwa chanzo cha kukamatwa ni baada Wamiliki wa shule
binafsi kwenda shuleni Lucky Vicent kutoa michango ya Rambirambi
shuleni Lucky Vicent
Habari zinasema kuwa kwa sasa Watu wote waliokamatwa tayari wamefikisha kituo cha kati kilichopo mjini Arusha (Central)
Waliokamatwa kwenye msafara huo wanatajwa ni wanahabari 10, Mmiliki wa shule ya Lucky Vicent na Meya Kalist Lazaro.
Waandishi
waliokamatwa ni pamoja na 1 .Godfrey Thomas ayo tv 2.Alphonce kusaga
Triple A 3.Filbert Rweyemamu mwananchi 4.Husein Tuta Itv 5.Joseph
Ngilisho Sunrise radio 6.Geofrey Steven Radio 5 7.Janeth Mushi Mtanzania
8.Zephania Ubwani The Citizen 9.Elihuruma Yohani mwakilishi wa Tanzania
Daima 10.Idd uwesu Azam Tv
Post a Comment