Manji Aripoti Kituo Kikuu cha Polisi, Dar
MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga na Diwani wa Kata ya Mbagala kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Manji, ameripoti leo Alhamisi Februari 09, 2017 saa 4:54 katika Kituo Kikuu cha Polisi kufuatika wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Yusuf Manji akiwa amezungukwa na wanahabari
Katika Orodha ya majina 65 yaliyotajwa na Paul Makonda hapo jana jina la Yusuf Manji lilikuwa miongoni mwa majina hayo na kutakiwa kuripoti siku ya Ijumaa ili kufanya mahojiano kuhusu tuhuma za kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.
Manji ambaye pia ni Mwenyekitu wa Klabu ya Yanga jana alizungumza na waandishi wa habari na kusema hatoweza kufika kituoni hapo siku ya Ijumaa.
Manji amefika kituoni hapo akiwa na wanasheria wake 8 ambapo wanasheria 6 ni raia wa Tanzania na wanasheria wawili ni raia wa Uingereza. Aidha, mashabiki wa Yanga wamejitokeza kwa wingi kituoni hapo kumuunga mkono kiongozi wao.
Mbali na Manji, wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Pamoja na Fremaan Mbowe, Askofu Josephat Gwajima, Iddi Azan.
Post a Comment