BARCELONA YATINGA KWA KISHINDO NUSU FAINALI YA COPA DE REY

  Denis Suarez akiachia shuti la umbali wa yadi 16 na kufunga goli la kwanza
 
Timu ya Barcelona imeibuka na ushindi wa magoli 5-2 dhidi ya Real Sociedad na kutinga nusu fainali ya kombe la Copa de Rey kwa ushindi wa jumla wa magoli 6-2.

Barcelona ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa Denis Suarez aliyegongeana vyema pasi na Luis Suarez na kisha baadaye Neymar akaangushwa na kuzaa penati iliyofungwa na Lionel Messi.

Luis Suarez aliongeza goli la tatu dakika moja tu kupita baada ya Juanmi kuifungia Real Sociedad goli la kwanza na Da Silva aliifungia Sociedad goli la pili kabla ya Turan kufunga goli la tano la Barcelona.
  Neymar akiwa amechezewa madhambi na beki Martinez na kusaidia kupatikana kwa penati
  Luis Suarez akimalizia kilaini pande alilopewa na Lionel Messi na kufunga goli.
                                          messi na Suarez wakimpongeza denis.

No comments

Powered by Blogger.