SITTA ALICHANGIA KIPIGO CHA MABAO 5-0 ILICHOPEWA YANGA

SPIKA wa zamani wa bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania, Samuel Sitta ameagwa jana jiji Dar es Salaam na bungeni Dodoma ambapo mazishi yake yanafanyika leo Jumamosi nyumbani kwao Urambo, Tabora.
Katika salamu za pole, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amemuelezea marehemu Sitta kuwa alitoa mchango mkubwa kwenye michezo hasa ndani ya klabu ya Simba kwani aliivusha kimataifa pamoja na kuhakikisha Wekundu hao wanaipiga Yanga bao 5-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom.
Zitto alisema kuwa Marehemu Sitta ameacha pengo kubwa kwenye michezo na atakumbukwa kwa mengi ndani ya Simba na wanamichezo wengine ambao alishirikiana nao."Marehemu Sitta atakumbukwa kwa namna alivyotoa mchango wake wa kuifunga Yanga bao 5-0, aliisadia kufikisha Simba hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya kimataifa, ni pengo kubwa ameliachana," alisema Zitto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli jana aliongoza maelfu ya watu kuuaga mwili Marehemu Sitta katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa kwenye Ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma ulikopokelewa na Spika wa Bunge hilo, Joseph Ndungai.
Marehemu Sitta alipatwa na mauti hiyo nchini Ujerumani alikokuwa akipata matibabu yake akisumbuliwa na tatizo la tezi dume. Mwili wa marehemu uliwasili nchini jana Alhamisi.
credit boiplus.blog

No comments

Powered by Blogger.