Askari Ajipiga Risasi Kifuani, Afariki Dunia!
MTWARA: Askari wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mtwara, aliyetambulika kwa jina la PC Sengerama amefariki
dunia baada ya kudaiwa kujipiga risasi ya moto kifuani leo majira ya
alfajiri wilayani Tandahimba mkoani humo.
Inadaiwa kuwa wakati askari huyo anafanya hivyo alikuwa katika lindo kwenye Benki ya NMB, Tandahimba.
Mwili wa marehemu ukiwa kwenye gari la polisi.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia
ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Henry Mwambambe
amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema bado hawajafahamu chanzo
cha askari huyo kujiua.
“Ni kweli kama mlivyosikia, askari
huyo amefariki dunia alfajiri ya leo kwa kujipiga risasi, lakini bado
hatujafahamu nini chanzo cha kujiua.
“Jeshi la Polisi linaendelea uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo, taarifa zikipatikana zenye ufasaha tutawaambia,” amesema Kamanda Mwambambe.
Taarifa zingine zilizotufikia hivi punde
zimeeleza kuwa, mwili wa marehemu umesafirishwa leo kupelekwa nyumbani
kwao mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi.
Post a Comment