RAIS BARACK OBAMA AKUTANA NA RAIS MTEULE DONALD TRUMP IKULU
Rais Mteule wa Marekani Donald Trump
amekutana na rais Barack Obama Ikulu katika mkutano uliolenga kuandaa
mazingira mazuri ya kukabidhiana madaraka.
Mkutano huo ambao ulilenga kumaliza
tofauti zao baada ya kampeni kuisha umemalizika kwa mafanikio makubwa
huku Trump akimuelezea rais Obama kama mtu mzuri.
Trump pia ametumia akaunti yake ya
twitta kutwitti kueleza kuwa alikuwa na wakati mzuri alipofika mara
ya kwanza Ikulu na kusema kuwa mkewe Melania amevutiwa na Michelle
Obama.
Melania Trump akimsikiliza Michelle Obama walipokutana Ikulu
Post a Comment