Filamu ya Wema na Van Vicker ‘Day After Death’ kuzinduliwa Valentine’s Day

Baada ya kiu ya muda mrefu kwa mashabiki wa filamu wa Wema Sepetu hatimaye mwigizaji huyo amesema filamu yake na mwigizaji wa Nigeria, Van Vicker ‘Day After Death’ itazinduliwa Valentine’s Day.
Malkia huyo wa filamu ambaye amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia filamu, amesema tayari filamu hiyo imekamilika na kinachosubiriwa ni uzinduzi tu.
“Nina movie yangu mpya na Van Vicker inakuja na nitaifanyia uzinduzi Valentine’s Day kwa sababu ni movie ya mapenzi,” Wema aliiambia Clouds TV.
Kwa sasa mwigizaji huyo anafanya matamasha mbalimbali ya ‘Usiku wa Vigoma’ ambayo yanaambatana na uzinduzi wa bidhaa zake mpya.

No comments

Powered by Blogger.