Askari Polisi watatu wafukuzwa kazi Mwanza
Jeshi
la polisi mkoani MWANZA limewafukuza kazi askari watatu kwa tuhuma za
kukiuka maadili ya kazi ikiwemo kujihusisha na vitendo vya uhalifu.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa MWANZA, AHMED MSANGI amesema kuwa uamuzi huo
umechukuliwa na jeshi hilo ili iwe fundisho kwa askari wengine ambao
hawazingatii weledi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumza
na Watendaji wa Jeshi la polisi mkoani MWANZA wakati wa kikao cha kazi
kilichofanyika kufuatia ongezeko la matukio ya ukiukwaji wa maadili
miongoni mwa baadhi ya Watendaji hao, Kamanda MSANGI amesema vitendo
hivyo havivumiliki.
Kamanda
MSANGI ametumia kikao hicho kuwakumbusha Watendaji wa Jeshi la Polisi
mkoani MWANZA kuzingatia weledi wakati wa kutekeleza majukumu yao na
kufanya kazi zao bila kumuogopa wala kumuonea mtu yoyote.
Post a Comment