WAMALAWI WAULIZANA YUPO WAPI RAIS WAO PETER MUTHARIKA
Wananchi wa Malawi wameanzisha
kampeni ya kuuliza kama kuna mtu yeyote anayejali kujua alipo rais
wao Peter Mutharika.
Rais Mutharika ambaye amekuwa rais
wa taifa hilo tangu Mei 2014, alisafiri kwenda kwenye Mkutano Mkuu wa
71 wa Umoja wa Mataifa Jijini New York.
Mkutano huo uliisha Septemba 26 na
karibu wakuu wote wa nchi waliohudhuria mkutano huo wamerudi kwenye
mataifa yao lakini Mutharika hajarudi.
Hali hiyo imewafanya Wamalawi kuja
na hashtag ya #BringbackMutharika, huku wakiikosoa serikali kwa
kuficha ukweli kuhusu afya ya Mutharika.
Post a Comment