Bondia Thomas Mashali Adaiwa Kuitiwa Kelele za Mwizi, Auawa kwa Kipigo!

DAR ES SALAAM: Bondia Thomas Mashali maarufu kama ‘Simba Asiyefugika’ ameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kupigwa na watu wasiojulikana baada ya kudaiwa kuitiwa kelele za mwizi, maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam, Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (TPBO), Yassin Abdallah amethibitisha.
 Thomasi Mashali akiwa katika Pozi uku akiwa na mkanda wake wa Ubingwa wa Taifa unaotambuliwa na TPBO

Mashali aliyezaliwa kwa jina Christopher Fabian Mashale, inasemekana wakati akinywa pombe, ulizuka ugomvi na mtu mmoja ambaye anadaiwa kupiga kelele kusema Mashali ni mwizi na watu kuanza kumshambulia.
 Mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali wakitunishiana misuli baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kupambana katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam wakati wa Tamasha la Matumaini Siku ya Sikukuu ya Nanenane (Agosti 8, 2014) lililoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers.
Ndugu zake wanadai kuwa walimkuta akivuja damu nyingi sehemu mbalimbali za mwili wake.
Taarifa zinadai kuwa alipelekwa katika Hospitali ya Sinza Palestina kabla ya kupelekwa Muhimbili ambako mauti yalimkuta.

 Bondia Thomas Mashali akizichapa na Bondia Francis Cheka (SMG) Sikukuu ya Krismasi Uwanja wa Jamhuri Morogoro, mwaka 2015.

Inasemekana kuwa hadi jioni alikuwa na bondia mwenzake, Francis Cheka.

No comments

Powered by Blogger.