KIKWETE AKAGUA VIFAA NA ENEO MAALUMU KWA WAGONJWA WA EBOLA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wauguzi waliovalia mavazi
maalumu tayari kutoa huduma kwa abiria atayekutwa na ugonjwa wa ebola
mara atapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea
Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo wakati alipokagua wodi
maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo
la hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam leo
Baadhi ya wahudumu waliovalia mavazi maalumu wa wodi maalumu
iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la
hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaangalia wahudumu waliopata mafunzo
maalumu ya kumhudumia mgonjwa wa ebola wakati alipokagua wodi maalumu
iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la
hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam leo
Post a Comment