LEBRON AMUINGIZA MWANAYE SHULE
Staa wa mchezo wa kikapu Marekani, LeBron James.
STAA wa mchezo wa kikapu Marekani, LeBron James, amekuwa na mapumziko maalum baada ya kuanza kazi ya kumfundisha mwanaye mchezo wa kikapu.
LeBron pamoja na wachezaji wengine walioshiriki NBA, wapo mapumzikoni kwa sasa wakisubiri msimu mpya wa Ligi ya NBA unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.
Lakini huku wachezaji wengine wakiwa kwenye fukwe mbalimbali, staa huyo yeye yupo na mwanaye kwenye kambi ya mazoezi ya AAU akimfundisha mchezo huo.
Pamoja na kwamba James amekuwa akifanya mazoezi na mastaa wengine kama Derrick Rose na Eric Bledsoe, lakini amekuwa akitumia muda mwingi sana kuhakikisha mwanaye anakuwa fiti sana kwenye mchezo wa kikapu.
Kinda huyo anayejulikana kwa jina la LeBron James Jr, ana umri wa miaka 12 lakini amekuwa akielezewa kuwa ni mchezaji mwenye kipaji cha juu sana.
Kinda huyo amekuwa akiitumikia timu ya watoto ya North Coast Blue Chips ambayo juzi ilicheza mchezo wa kirafiki na Oakland Soldiers ambapo James ndiye alikuwa kocha na timu hiyo ikalala kwa pointi 54-51.

Post a Comment