KIPA DIDA APIGA KONA HEWANI, AREJEA YANGA

Wakati ikiaminika kuwa kipa Deogratius Muishi ‘Dida’ yupo njiani kwenda nje kucheza soka la kulipwa huku wengine wakisema anaweza kuelekea Singida United, kipa huyo amerejea ndani ya Yanga.
Dida ambaye hakuwa katika mazoezi ya pamoja na wenzake, jana alikuwa mmoja wa wachezaji waliofanya mazoezi kwenye mazoezi ya gym akiwa na mastaa wengine wa Yanga na hivyo kufanya tetesi za kuwa anataka kuondoka hapo kuwa katika kizungumkuti.
Dida hakutaka kuzungumzia zaidi juu ya usajili wake lakini bado haijafahamika kama ndiyo karejea moja kwa moja au la, kwa kuwa hata baadhi ya watu wa ndani wa Yanga walishanukuliwa wakisema kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Simba na Azam FC yupo njiani kuondoka.

No comments

Powered by Blogger.