KESI YA MANJI YAAHIRISHWA, AENDELEA KUTIBIWA MUHIMBILI

                                                           Yusuf Manji.
KESI inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji imeahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jiji Dar hadi Agosti 4 mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.
Kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu, Huruma Shaidi ilikuwa isikilizwe leo lakini Manji hakufika mahakamani hapo kwa kile kilichoelezwa na mawakili wake kuwa ni mgonjwa na yupo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Muhimbili akitibiwa maradhi ya moyo.

Julai 5 mwaka huu, Manji akiwa amelazwa Muhimbili alisomewa mashtaka saba na watuhumiwa wenzake, yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe, plate number mbili za magari ya serikali jambo ambalo nalo ni kinyume cha sheria.
Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mtu mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja na wote wamerudishwa rumande.

No comments

Powered by Blogger.