‘Tutapoza machungu kwa Mbao FC’ – Kocha wa Simba SC

                                                   Kocha wa Simba SC ‘Joseph Omog’
 
Kocha wa Klabu ya Simba, Joseph Omog amekubali yaishe kuhusu ubingwa wa Ligi Kuu vodacom Tanzania Bara na kuahidi kuwa Klabu yake itapoza machungu kwa kuchukua ndoo ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Mbao FC ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.
Klabu ya Simba SC imenyang’anywa tonge mdomoni na wapinzani wao Yanga SC kwa tofauti ya magoli tuu! huku wote wakiwa na pointi 68,Ingawaje bado Uongozi wa Simba unadai hautambui ushindi wa Yanga mpaka rufaa yao walipeleka FIFA itakapotolewa majibu .
“Kila mmoja ameona jinsi ambavyo tulipambana tangu mwanzo wa ligi mpaka mwisho wake ambapo tumekosa ubingwa kwa tofauti ya mabao pekee, lakini nia yetu ilikuwa ni kuutwaa ubingwa ili tujikatie nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, Lakini hiyo siyo kitu kwa sababu licha ya kukosa kwa njia hiyo ya kuchukua ligi, kwa sasa tuna mechi ya fainali mkononi ambayo hiyo tunataka kuitumia kwa ajili ya kupoza machungu yetu ya kukosa ubingwa lakini pia kujipatia nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa ambapo mara ya mwisho ilikuwa miaka mitano nyuma,”Alisema Omog kwenye mahojiano yake na Gazeti la Championi.
Simba SC itavaana na Mbabe wa Yanga SC  ‘Mbao FC’ kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho litakalofanyika huko mkoani Dodoma kunako Dimba la Uwanja wa Jamhuri tarehe 24 Mwezi huu na kama Simba wakishinda basi watapata nafasi ya kushiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

No comments

Powered by Blogger.