MANCHESTER UNITED HATARINI KUTUPWA NJE LIGI YA UROPA

 Timu ya Fenerbahce imefunga mara mbili magoli mazuri dhidi ya Manchester United na kukifanya kikosi hicho cha Jose Mourinho kuwa hatarini kuondolewa katika Ligi ya Uropa.
 
Mshambuliaji Moussa Sow aliipatia Fenerbahce goli la kuongoza katika sekunde ya 65 kwa kufunga kwa tik taka na kisha Jeremain Lens kufunga goli la pili la mpira wa adhabu.

Katika mchezo huo Manchester United ilishuhudia Paul Pogba alitoka nje baada ya kuumia, hata hivyo baadaye Wayne Rooney alifunga goli pekee kwa timu yake kwa shuti la yadi 25.
            Moussa Sow akifunga goli la kwanza katika mchezo huo kwa tik taka
                      Jeremain Lens akishangilia goli lake alilofunga kwa kukimbia

No comments

Powered by Blogger.