Serikali yamrudisha kazini Mkurugenzi waliyemtumbua
Serikali
imerejesha kazini Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya pamba Tanzania Bwana Marco
Mtunga baada ya kushindwa kupata uthibitisho wa tuhuma zilizokuwa
zikimkabili za matumizi mabaya fedha kiasi cha shilingi bilioni 2.4
zilizotakiwa kulipwa wakulima wa pamba walioathirika na mdororo wa
uchumi wa mwaka 2008.
Akizungumza
na waandidhi wa habari waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi, Mhe Dkt
Charless Tizeba pichani amesema Bwana Mtunga anakiwa kuripoti ofisini
katika nafasi yake kuanzia sasa na kusisitizia serikali imejiridhisha
tuhuma zilizokuwa zikimkabiri hazina ukweli wowote.
Aidha
siku cha chache baada ya waziri kuu kuagiza kufanyika mabadiliko katika
ya bodi ya Korosho, hatimaye serikali imemuondoa Kaimu Mkurugenzi wa
bodi ya Korosho Bwana Mfaume Mohamed, na kaimu mkurugenzi wa masoko
Bwana Juma Yusuf na kuwateua bwana Hassani Jarafu kuwa kaimu mkurugenzi
mkuu wa bodi hiyo, pamoja na bwana Ray Mtangi kuwa kaimu mkurugenzi wa
masoko, na kuwabadilisha wajumbe wote wa bodi.
Mhe
Dkt Tizeba amesema serikali ya awamu ya tano inaendelea kuboresha
utendaji katika maeneo mbalimbali ili kuongeza tija na ufanisi,pamoja na
hatua kubwa ambazo zimefikiwa katika sekta ya korosho serikali bado
inaamini kuwa inaweza kufanya vizuri zaidi, ambapo sasa bei ya korosho
imepanda hadi kufikia shilingi elfu tatu na mia sita kwa kilo, huku
pamba pamba ikiwa imefikiwa shilingi elfu tatu na mia tatu kiwango
ambachi hakijawahi kufikiwa toka kilimo cha korosho na kuanza hapa
nchni.
Post a Comment