MANJI ASEMA MAANDALIZI YA MKUTANO SAFI, ULINZI UMEIMARISHWA, WANACHAMA WAJITOKEZE MAPEMA NA WAWE HURU

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameomba wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa dharura alioitisa keshokutwa Jumapili.

Manji pia amewaomba wanachama hao kuwahi saa mojaa subuhi ili wapate nafasi ya kusema mambo kadhaa watakayojadili kwa uafasaha ili wawe na uelewa wa kutosha wa nini wanachojadili na kama kuna mtu hajaelewa, awe huru kuuliza.

“Tufike mapema, litakuwa ni jambo zuri zaidi. Kila mtu atapata nafasi ya kusema tunakwenda kuzungumza nini. Kama kuna ambaye hajaelewa, basi ni vizuri akauliza na kupewa ufafanuzi pale.

“Tuwe huru kujua tunachotaka kuliko kukaa kimya kwenye mkutano na baadaye kwenda kuanza kuzungumza pembeni,” alisema.

Aidha, kuhusiana na suala la ulinzi, Manji alisema maandalizi ya mkutano yanakwenda vizuri likiwemo suala la ulinzi.

Alisema ulinzi umeimarishwa na utakuwa na uhakika na hakuna haja ya mtu kuwa na hofu kwamba huenda kutakuwa na vurugu.

Kuhusiana na suala la kukodisha, Manji alisema watu watakuwa huru na kulichambua na wameamua kuitisha mkutano huo ili kutimiza agizo la serikali la kwamba mkutano wa kwanza ulikuwa na mapungufu.


Kuhusiana na wanachama ambao hawajalipa ada, Manji aliwashauri kufanya juu chini walipe ada zao ili kupata nafasi ya kushiriki mkutano huo ambao unasubiriwa na wanachama wengi wa klabu hiyo pamoja na mashabiki ili kujua hatma ya klabu yao kuhusiana na suala la kukodisha na mambo mengine ya maendeleo.

No comments

Powered by Blogger.