Davido Awapigia Magoti Wanigeria
STAA wa muziki wa Nigeria, Davido (pichani juu) amewaomba Wanigeria
kumpa muda rais wa nchi yao, Muhammadu Buhari kutokana na hali mbaya ya
kiuchumi inayoikabili nchi hiyo, ambapo amewaomba wampe muda atairejesha
nchi sehemu nzuri.
Muhammadu Buhari.
Davido, baba wa mtoto mmoja, amesema anaamini Buhari ni kiongozi
mzuri lakini anahitaji muda kuiweka nchi sehemu nzuri kiuchumi. Kwa sasa
nchi hiyo imekuwa ikikabiliwa na hali ngumu ikidaiwa kuwa uchumi wake
umeshuka na kusababisha mzunguko wa fedha kuwa mdogo pia.
Post a Comment